Psalms 38:3-7

3 aHakuna afya mwilini mwangu
kwa sababu ya ghadhabu yako,
mifupa yangu haina uzima
kwa sababu ya dhambi zangu.
4 bMaovu yangu yamenifunika
kama mzigo usiochukulika.

5 cMajeraha yangu yameoza na yananuka,
kwa sababu ya upumbavu wa dhambi zangu.
6 dNimeinamishwa chini na kushushwa sana,
mchana kutwa nazunguka nikiomboleza.
7 eViuno vyangu vimejaa maumivu yaunguzayo,
hakuna afya mwilini mwangu.
Copyright information for SwhNEN